Burudani

MB Dog: Ngoma zinatoka kibao, wasikilizaji walewale, utahit vipi?

Hitmaker wa ‘Latifa’ MB Dog amezungumza na Bongo5 sababu ya nyimbo nyingi za wasanii kutofanya vizuri na kudai kuwa muziki wa sasa unahitaji nguvu nyingi ili uweze kufika mbali.

MBDogg

“Watu sasa hivi wakitoa ngoma inakuwa kama shida vile, kwa sababu unakuja ndani ya wakati mmoja kuna ngoma nyingi zimetoka. Wasikilizaji ni wale wale na redio ni zile zile. Kwa mfano hii ngoma niliyofanya na Q Chillah, nimeshangaa Zanzibar imefanya vizuri zaidi ya hapa. Kwahiyo muziki wa sasa hivi unahitaji nguvu nyingi sana ili uweze fika mbali. Lakini kwa hatua tuliyofikia na wimbo wetu sio mbaya kwa sababu tulikuwa tunaangalia hali huko ikoje. Kwahiyo ujio wetu mpya tutajipanga vizuri zaidi.”

Katika hatua nyingine MB Dog amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula na ujio wa wimbo mpya uitwao Bado Bado.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents