Burudani

Young Dee kuja na ‘reality show’ ya TV kwaajili ya mashabiki wake

Rapper Young Dee anatarajia kuja na reality show yake mpya ya Tv hivi karibuni.

Young D

Young Dar es salaam ambaye yuko chini ya studio za Authentic amesema kipindi hicho kitakuwa na mambo yake yanayowahusu mashabiki wake.

“Kuna show yangu ambayo ni reality show ambayo tumeshaanza kuishoot,” ameiambia Global TV Online. “Itakuwa inazungumzia moments zangu nyingi ambazo hizo moments sana sana zinamhusu yule shabiki wangu wa ukweli , ambaye anampenda na anatamani sana kuwa anapata muda wake kuwa na Young Dee, kuona vitu gani anavyovifanya. So ni show kwaajili ya hawa mashabiki wangu kabisa.”

“So itaanza kuruka maybe ndani ya wiki hizi mbili tatu sababu tumeshaanza kuishoot na material yote iko tayari.”

Young Dee amesema kuwa watatoa taarifa rasmi ya kituo cha runinga ambacho kitakua kikionesha reality show yake mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents