Habari

Mbowe na wenzake, Halima Mdee wapata dhamana

Viongozi Sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamaeachia huru mara baada ya kutimiza masharti ya dhamana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Washtakiwa hao walitakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Tsh Milioni 20 na kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao wa vijiji au mtaa ambao watapaswa kuwa na nakala za vitambulisho vyao.

Viongozi hao waliopata dhamana ni  Freeman Mbowe, John Mnyika , Ester Matiko, Salum Mwalimu, Peter Msigwa na Dkt. Vicent Mashinji.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameunganishwa na  akina Freeman Mbowe ambapo alisomewa mashtaka mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kuendelea na mkusanyiko huo, kutotii amri iliyowataka kutawanyika na kusababisha vurugu iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwilini na askari kujeruhiwa.

Hata hivyo naye Mahakama imempa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini kwa maandishi bondi ya Sh milioni 20 na kuripoti mara moja kila wiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents