Habari

Mbunge aiomba serikali kumshughulikia Waziri wa Zanzibar aliyedaiwa kugoma kukaa karantini ya corona na kusababisha maambukizi kwa watu wawili

Mbunge wa Konde Nchini Tanzania (CUF) Khatib Said Haji ameiomba Serikali kumchukulia hatua Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib aliyekataa kukaa kwenye karantini na kusababisha maambukizi kwa watu wawili kwenye familia yake.

Akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 amesema matokeo ya Hilo nyumbani kwake kuna watu wawili amewaambukiza na huko hospitali haijulikani matokeo yake nini.

“Ndani ya siku tatu ameng’ang’ana kukaa hospitali ya Mnazi Mmoja matokeo yake akatolewa kwa nguvu baada ya kuona jambo hili limekuwa kubwa sana. Baada ya malalamiko makubwa ndio alikubali kuwekwa kwenye karantini,”amesema.

Amesema alifanya hivyo kwa sababu ya kiburi cha madaraka yake na kumpongeza makamu wa pilli wa Rais Zanzibar kwa kukubali kukaa karantini alipotoka nje ya nchi bila kulazimishwa.

“Huu ndio utu, huu ndio ubinadamu leo waziri huyu ni nani anayekataa uamuzi wa Serikali hata uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatuwezi kumchekea mtu mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu ni waziri ulichukulie hatua haraka. Leo hii baada ya kiburi kingine kuna mtu mwingine ni daktari anaitwa Hafidh hadi leo ameng’ang’ana pale Hospitali ya Mnazi mmoja kwa sababu ana unasaba wa kiukubwa.”

“Uheshimiwa wake ni kwa sababu ana uhai anapumua dakika moja akifumba macho anakuwa marehemu. Taharuki iliyopo pale Mnazi mmoja baada ya matukio hayo ni kubwa. Nataka mheshimiwa ufuatilie kama huyu daktari bado yupo,”amesema.

Amesema kauli anazozitoa katika mtandao ya jamii ni utasema hakuna yoyote anayeweza kumfanya lolote.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali ilimuondoa kwa nguvu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib katika Hospitali ya Mnazi mmoja na kumuweka karantini.

Akihitimisha hotuba ya Bajeti ya Ofisi yake leo bungeni, Majaliwa amesema awali Waziri huyo alikataa kukaa karantini

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents