Habari

Mch. Peter Msigwa mikononi mwa Polisi

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kutokana na matukio ya kiuharifu yanayotokea mjini Iringa.

Mbunge huyo anahojiwa kuhusu kuchomwa nyumba ya Katibu wa UVCCM na kuvunjwa Nyumba ya Diwani aliyehamia CCM akitokea CHADEMA.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Julius Mjengi ameuthibitisha kushikiliwa kwa Mchungaji Peter Msigwa ambapo ameeleza anahojiwa kuhusu  matukio ya uvunjwaji wa nyumba ya aliyekuwa diwani wa kata ya Mwangata kupitia chadema aliyejiuzulu na kujiunga na CCM pamoja na tukio la kuchomwa moto kwa nyumba aliyokuwa akiishi katibu wa UVCCM Iringa mjini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents