Michezo

Mchezo wa marudiano dhidi ya Cameroon utakuwa mgumu – Shime

Kocha wa Serengeti Boys, Bakari Shime, ameelezea hisia zake za mchezo wao wa kwanza dhidi ya Simba wa nyika, kikosi cha Cameroon kabla ya kukutana tena katika mchezo wa marudiano siku ya Jumatano.

“ Hongera sana kwa vijana wetu kwa kazi nzuri sana ambayo wanaifanya kwa kufuata maelekeza ya waalimu. Mchezo uliopita ulikuwa mgumu, mwenye ushindani na Ufundi mwingi. Cameroon walituzidi sana kwenye upande wa physical na wana wachezaji ambao wana maumbo makubwa tofauti na wa kwetu, lakini kimsingi vijana walikaa imara na waliweza kuhimili kila aina ya vitimbi vya Cameroon. Mechi ya pili itakuwa ngumu zaidi kwakuwa wao wameona Ubora wetu na udhaifu wetu”.

Mfungaji wa Bao pekee la Serengeti Boys, Ally Hamisi Ng’azi, ameelezea namna alivyouona Mchezo wa kwanza. “Mchezo uliopita ulikuwa Mgumu hasa katika kipindi cha kwanza kwa kuwa walikuwa wanausoma Mchezo na wao walikuwa wakiwasoma pia. Goli lake ni kutokana na kufuata maelekezo ya mchezo”

Wakati goli kipa aliyekuwa amesimama katika mtamba wa Panya katika mchezo huo Ramadhani Awam kabwili maarufu kama Kaseja amekiri kila mchezo kwao ni kama fainali

“Wao wanahitaji kushinda kila mchezo na wamejiandaa vizuri kutoka Morocco na hivyo watanzania wajiaandae kuwapokea kwao wakiwa na Kombe la Dunia. Kuwafunga Cameroon si kazi rahisi, kwani wao ni wazuri hasa katika uwanja wao wa nyumbani”.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents