Burudani

Mtanzania aishiye ujerumani, aachia video hii ya dance

Emanuel Austin, mtanzania ambaye ni mwalimu wa dance (choreographer) mwenye chuo maarufu nchini Ujerumani [Emanuel Austin & Larissa Bertsch], amekuletea video ya Hip Hop dance. Video hiyo imechezwa na wanafunzi takribani 20 kutoka katika chuo chake.

Akiongea na Bongo5, mwalimu huyo ambaye pia anamiliki lebo ya EMA ENTAREIMENT nchini humo, amesema baada ya kuachia choreography hiyo, ataenda na wanafunzi wake hao walioshiriki kwenye video hiyo katika mashindano ya kucheza ya Germany Championship, yatakayofanyika mjini Hannover Juni 5 mwaka huu.

Wakati huo huo Austin ameongeza kuwa hivi karibuni ataachiwa wimbo wake mpya, baada ya ‘Mapenzi Digitali’ ,aliouachia miezi mitano iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents