Michezo

Mfahamu kiungo mahiri wa soka aliyefariki jana Ibrahim Rajab ‘JEBA’  na kauli ya Simba SC 

Mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Azam FC na Taifa Stars, Ibrahim Rajab ‘Jeba’ amefariki dunia jana katika hospitali ya Mnazi Mmoja visiwani Zanzibar.

Image result for Ibrahim Rajab ‘Jeba’

Wanasoka wengi walimfahamu akiwa kwenye kilele cha ubora wake wa soka alipokuwa pale ndani ya klabu ya Mtibwa Sugar na Azam FC. Jeba alikuwa mchezaji wa Chuoni FC.

Hakuzungumziwa sana wakati anaanza safari yake ya soka ndani ya ligi kuu kama wengine lakini alijua kutatua changamoto hizo ni kucheza kwa akili nyingi na maarifa ya hali ya juu.

Image result for Ibrahim Rajab ‘Jeba’

Ndipo Ibrahim Rajab ‘Jeba’ akang’ara sana kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi Zanzibar na Ligi Kuu nzima ya Tanzania Bara.

https://www.instagram.com/p/B2lPDhpn8Zk/

Kiungo fundi katika soka la Tanzania uliyefariki dunia siku moja na kiungo mwenzako wa zamani wa klabu ya Rangers ya Scotland na timu ya taifa ya Uholanzi, Fernando Recksen. Inna lilah wainna ilaih rajiun, Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents