Habari

Mfahamu msemaji mpya wa Serikali Makoba

Thobias Makoba, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali. Makoba anachukua nafasi ya Mobhare Matinyi ambaye amepangiwa majukumu mengine. Kabla ya Uteuzi huu Bw. Makoba alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Majili wa Hazina.MFA

Kabla ya kujiunga na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Makoba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pamoja na kushiriki katika majukwaa mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo UN, African Union, SADC, EAC, World Economic Forum na mengineyo, kwa vipindi mbalimbali aliwahi kuwa Katibu wa Mawaziri wawili wa Mambo ya Nje Bernard Membe na baadae Balozi Dokta Augustine Mahiga kabla ya Kwenda kuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar.

Makoba ana Masters Degree in Security and Strategic Studies kutoka National Defence College – Tanzania, Post-Graduate Diploma in Economic Diplomacy kutoka Chuo Cha Diplomasia Kurasini na Degree ya kwanza ya Political Science and Sociology with majors in International Relations.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents