HabariMichezo

Mfungaji Bora wa NBC 2021/22 ni George Mpole

Mshambuliaji hatari wa Klabu ya Geita Gold, George Mpole amefanikiwa kumaliza Ligi Kuu leo Juni 29, 2022 akiwa na magoli 17 dhidi ya mpinzani wake Fiston Mayele mwenye mabao 16.

Mpole anayehusishwa na kusajiliwa Simba SC, amefunga goli hilo la 17 dakika ya 11 dhidi ya Coastal Union.

Kwa magoli hayo 17 ya Mpole dhidi ya mpinzani wake katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu Fiston Kalala Mayele mzee wa ‘Kutetema’ sasa hana mpinzani tena kutona na Ligi hiyo kutamatika leo.

Kwa msimu wa pili mfululizo Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara anakuwa Mtanzania, msimu wa 2020/22 alikuwa John Bocco magoli 16 na msimu huu wa 2021/22 ni George Mpole wa Geita Gold  mabao 17.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents