Mgao Wa Umeme Waisha

Juhudi za Wataalamu wa umeme kutoka marekani zimefanikisha kutengemaa kwa mtambo mmoja kati ya mitatu ya kuzalisha umeme wa megawati 40 amabyo iliharibika katikakati ya wiki iliyopita

Juhudi za wataalamu waliofika jana kutoka Marekani kutengeneza mtambo mmoja unaozalisha umeme wa megawati 40, zimefanikisha kutengemaa kwa mtambo huo na kulinusuru taifa kutoka katika adha ya mgawo wa umeme ulioanza katikati ya wiki iliyopita.

Akizungumza na wanahabari jana katika ofisi ya makao makuu ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa shirika hilo, Badra Masoud, alisema jitihada za mafundi hao waliofanya kazi usiku kucha, ziliwezesha kutengeneza moja ya mitambo mitatu iliyoharibika ghafla.

Kutokana na hali hiyo, TANESCO imetangaza kutokuwapo kwa mgawo wa umeme nchi nzima labda dharura ndogo ndogo ambazo shirika litatangaza endapo zikitokea.

“Kuanzia leo hakutakuwa na mgawo tena…wataalamu wamekwishatengeneza mtambo mmoja wa Songas unaozalisha megawati 40,” alisema Badra.

Kwa mujibu wa meneja huyo, kwa sasa Songas itakuwa inaipatia TANESCO megawati 112 badala ya 72 zilizokuwa zikitolewa siku nne zilizopita mitambo ile mitatu ilipoharibika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents