Habari

Miaka 10 maabara haijakamilika, Naibu waziri Silinde apigwa butwaa

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde ameagiza Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) kufanya ukaguzi wa ujenzi wa maabara tatu katika shule ya sekondari ya Nkome iliyopo halmashauri ya wilaya ya Geita baada kubainika gharama iliyotumika ni kubwa na ambayo haiendani na majengo ambayo bado hayajakamilika kwa zaidi ya miaka 10.

Maagizo hayo ameyatoa baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa maabara, ambapo fedha zilitolewa kupitia mpango wa huduma za jamii (CSR) na mgodi Gaita.

Katika taarifa iliyosomwa mbele yale ilionekana kutofautina na taarifa iliyotolewa na GGM kuwa maabara hizo zimekamilika kwa gharama ya milioni 86 wakati uhalisia unaonesha maabara hazijakamilika.


Naibu Waziri Silinde baada ya kukagua alitoa maelezo ya kuandikwa barua ya maelezo ya kina gharama za ujenzi kwenda kwa katibu mkuu TAMISEMI na nakala kwa Waziri na Naibu Waziri zifike ndani ya siku saba na ikiibanika kuna mtumishi wa serikali ameshiriki katika ubadhilifu wa fedha basi atarudisha fedha hizo na kuchukuliwa hatu za kisheria.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini Joseph Kasheku (king Msukuma) amemwambia Naibu waziri Silinde kuwa fedha za CSR kulingana na maelezo ya mgodi wa GGM ni kuwa maabara hizo zimekamilika lakini ukiangalia uhalisia wa jengo hali hailidhishi kabisa nakuomba serikali ingilie kati kusaidia umaliziaji wa maabara hizo ili wanafunzi waanze kutumia.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauli ya wilaya ya Geita Edith Mpinzile alimueleza Naibu Waziri kuwa walipokea vifaa vyenye thamani ya zaidi milion 47 kutoka GGM na milion 20 ambayo walitoa kwa fedha za makusanyo ya ndani na wananchi wa Nkome walitoa milion kwa kuanza ujenzi wa boma lakini makadirio ya ujenzi wa mabaara hizo tatu ambazo upo katika mkataba ni milioni 86.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents