Burudani

Miriam Ntakisivya mrembo wa Bongo aliyebarikiwa vipaji vingi anayetabiriwa kufanya makubwa

Tasnia ya burudani Bongo imezidi kupanuka na kufanya vizuri kwenye nchi mbalimbali za Afrika na duniani kiujumla. Miriam Ntakisivya ambaye ni designer, video vixen na msanii wa Bongo Flava ni mmoja kati ya watu ambao wanatabiriwa kuja kufanya makubwa.

Mrembo huyo ambaye kwenye mtandao wa Instagram anatumia jina la @Riam_Ntakisivya amefanikiwa kuingia mkataba na kampuni kubwa ya nchi Burundi Kora Entertainment ambayo itakuwa ikisimamia kazi zake nchini humo pamoja na nchi nyingine za jirani. Na kwa kuanza Riam ametumika kama model kwenye video ya wimbo wa msanii wa Burundi ‘Too Much’ ambaye anafahamika kama Sat-B.

Riam ameiambia Bongo5 kuwa anatarajia kufanya makubwa kupitia kampuni hiyo kwakuwa kwa sasa amejikita rasmi kwenye tasnia ya muziki.

“Mwanzo nilikuwa sipo serious sana kwenye upande huu lakini kwa sasa nimeingia rasmi kwakuwa nimeingia mkataba na kampuni ya Kora Entertainment ambayo itakuwa inasimamia kazi zangu nchini Burundi na nchi nyingine za jirani. Kwa upande wa Bongo nipo chini ya Mo Fire Again ambayo inamilikiwa na Mo Fire. Natarajia kufanya makubwa na kwa sababu ngoma yangu inayofuata watasikika wasanii wakubwa wa Bongo ambao nimewashirikisha,” amesema Riam.

“Nilistop kidogo kwenye kazi ya video vixen kwa sababu wasanii walikuwa hawajaijua thamani yetu,” ameongeza. Mrembo huyo pia ameshawahi kuonekana kwenye video kadhaa za Bongo ikiwemo ‘Yule Yule’ ya PNC na nyingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents