Michezo

Misri wa tinga fainali za Afcon Gabon

Timu ya taifa ya Misri imeafanikiwa kufuzu kutinga kwa mara ya tisa katika fainali za kombe la Afrika baada ya kuishinda Burkina Faso 4-3 katika mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1.

Mlinda lango wa miaka mingi Essam El Hadary alithibitisha ushujaa wake kwa kuokoa penalti iliopigwa na Betrand Traore ili kupata ushindi huo.

Wakati wa muda wa kawaida Mohamed Salah aliiweka kifua mbele Misri baada ya kufunga bao zuri.

Hatahivyo Burkina Faso walisawazisha wakati Aristide Bance alipofunga krosi iliopigwa na Charles Kabore.

Kupitia bao hilo Burkina Fasso imekuwa timu ya kwanza kuifunga Misri katika mchuano huo.

Wachezaji wa Burkinabe walioonyesha mchezo mzuri wakati wa muda wa kawaida walianza penalti hizo kwa kufunga, lakini Misri ikaibuka mshindi baada ya Traore kushindwa kucheka na wavu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents