Habari

Mkali wa Gangsta’s Paradise Coolio apoteza maisha akiwa na miaka 59

TMZ inaripoti kuwa Msanii Coolio Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59. Coolio amefia nyumbani kwa rafiki yake mjini Los Angeles walipoenda kumtembelea.

Kwa mujibu wa taarifa za awali wanasema, Coolio alienda bafuni na alivyochelewa kutoka, rafiki huyo alianza kumwita, na hatimaye akaingia bafuni na kumkuta Coolio akiwa amejilaza sakafuni.

Watu wa huduma ya kwanza walifika eneo hilo na kuripoti kuwa amefariki, wahudumu wa afya wametoa repoti ya kwanza ambayo inasema labda amefariki baada ya kupata mshtuko wa moyo. Sababu rasmi ya kifo haijabainishwa.

Coolio, ambaye jina lake halisi ni Artis Leon Ivey Jr ni rapa maarufu duniani, anatoka L.A. , mwaka 1995 alitingisha dunia na rekodi yake ya “Gangsta’s Paradise” ambayo ilitumika kwenye filamu ya Michelle Pfeiffer, “Dangerous Minds”, wimbo huu ulishika nafasi ya kwanza kwenye billboard na kukaa kwa wiki 3. #Bongo5Updates

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents