Burudani

Mkojo wa Wema Sepetu wakubalika mahakamani

Kesi ya malkia wa filamu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili wanayotuhumiwa kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya aina ya Bangi imeendelea kusikilizwa tena Ijumaa ya leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hakimu ambaye anayesikiliza kesi hiyo, Thomas Simba amekubali ushahidi wa vielelezo wa vipimo vya mkojo wa Wema ambao ulitolewa Jumatatu hii mahakamani hapo na upande wa serikali kutoka kwa Mkemia Mkuu ambapo upande wa washtakiwa kupitia wakili wao Peter Kibatala waliupinga ushahidi huo kutokana na kukiuka baadhi ya sheria na kukosekana kwa fomu muhimu ya kuambatanishia.

Kwa upande wa washatakiwa leo walikuwa wakisimamiwa na mwanasheria Tundu Lisu pamoja na mawakili wengine wawili huku kwa upande wa serikali kesi hiyo inasimamiwa na wakili Constantine Kakula.

Hata hivyo kesi hiyo imesogezwa mbele kutokana na mashahidi wengine wa upande wa serikali kushindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kupata dharula.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena August 15 na 16 ya mwaka huu. Wakati huo huo Hakimu Simba amesisitiza kuwa kesi zote zilizokaa muda mrefu mahakamani zinatakiwa kufanyiwa haraka kumalizika pamoja na zile kesi ambazo zinaonekana kuwa na mvuto mkubwa kwa watu ili kuondoa msongamano mkubwa mahakamani hapo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents