Burudani

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awataka wasanii kuanzisha taasisi za fedha

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki amewataka wasanii wa muziki na filamu nchini kujianzishia tasisi zao fedha ili waweze kufanya biashara kutokana na pesa zao wenyewe.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akizungumza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akizungumza na mamia waliojitokeza kumuaga marehemu George Tyson

Akizungumza jana na wasanii wa filamu na muziki pamoja wadau mbalimbali waliojitokea kumuaga aliyekuwa mtayarishaji wa filamu na vipindi vya TV, marehemu George Tyson, mkuu huyo wa mkoa aliwataka wasanii kuacha kutumia pesa zao kwa mambo mabaya.

“Mnaweza kwa kuanza kuanzisha Saccos polepole mnaweza mkafika mahala mkajenga uwezo wa kifedha ambao utawawezesha kuweza kufanya kazi kubwa zaidi, na mimi nina uhakika mkifanya hivyo mtaweza. Vijana wengi siku hizi hawa wa bongomovie, hawa wa bongoflavA wana uwezo wa kifedha lakini tunakimbilia kufanya yale mambo yasiyo ya msingi, tunakimbilia kufanya mambo ya starehe, tunakimbilia utambuliwe na mara nyingine mnatambuliwa kwa mabaya si kwa mazuri, si kwa uadilifu kitu ambacho kinakupotezea sifa. Unatumia fedha, kwanini fedha hizo mesizilekeze katika kujenga umoja thabiti ambao utawaimarisha kifedha na hatimaye mkafanya kazi iliyo nzuri,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents