Burudani

Orodha ya nominees walioingia nne bora ya tuzo za watu yatangazwa

Tarehe 20 May, Bongo5 Media Group ilitangaza majina matano yaliyopendekezwa kuingia kwenye tuzo za watu Tanzania kwa mwaka 2014 katika vipengele 11. Kwa wiki moja na siku kadhaa, wananchi wameshiriki kuwapigia kura watangazaji wa redio na TV wanaowapenda, vipindi vya redio na TV wanavyovipenda, video za muziki wanazozipenda, waigizaji na filamu wanazozipenda pamoja na wanamichezo.

background 2

Zoezi la upigaji kura limehusisha njia ya ujumbe mfupi wa simu pamoja na website. Na sasa mchujo wa kwanza umefanyika ambapo mshiriki mmoja katika kila kipengele ambaye amepata kura chache zaidi ametoka na hivyo kuwabakiza washiriki wanne watakaoendelea na kinyang’anyiro. Majina manne yanayoendelea yamepatikana kwa asilimia 100 za kura za wananchi.

Wiki moja baada ya mchujo huo wa kwanza, mchujo wa pili utafanyika tena na kuwabakiza wanaowania watatu kwenye kila kipengele. Tunawaomba washiriki waendelee kujipigia debe na kuwaomba mashabiki wao wawapigie kura bila kuchoka ili wajihakikishe nafasi ya kuingia fainali.

Wanaowania tuzo wote (watatu katika kila kipengele) waliosalia baada ya kufanyika mchujo wa pili na (wa mwisho), watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo, utakaofanyika wiki mbili baada ya mchujo huo wa pili, ili kutoa nafasi ya mashabiki wao kuendelea kupiga kura.

Kwenye hafla ya ugawaji tuzo hizi, kila mshindi atakayetangazwa, atapokea zawadi ya fedha taslimu, shilingi 1,000,000 za Kitanzania pamoja na tuzo ya thamani iliyotengenezwa kwa mkono kutoka kwenye mali ghafi za asili ya Kitanzania.

ORODHA YA NOMINEES WA TUZO ZA WATU WALIOINGIA NNE BORA

1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
1. Vanessa Mdee – Choice FM Andika TZW1 Vanessa kwenda 15678
2. Millard Ayo – Clouds FM Andika TZW1 Millard kwenda 15678
3. Hamis Mandi aka B12 – Clouds FM Andika TZW1 B12 kwenda 15678
4. Maryam Kitosi – Times FM Andika TZW1 Maryam kwenda 15678

2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
1. The Hitlist – Choice FM Andika TZW2 The Hitlist kwenda 15678
2. XXL– Clouds FM Andika TZW2 XXL kwenda 15678
3. Amplifaya – Clouds FM Andika TZW2 Amplifaya kwenda 15678
4. Hatua Tatu – Times FM Andika TZW2 Hatua Tatu kwenda 15678

3. MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
1. Salama Jabir – EATV Andika TZW3 Salama kwenda 15678
2. Sam Misago – EATV Andika TZW3 Sammy kwenda 15678
3. Zamaradi Mketema- Clouds TV Andika TZW3 Zamaradi kwenda 15678
4. Salim Kikeke – BBC Swahili Andika TZW3 Salim kwenda 15678

4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
1. Friday Night Live – EATV Andika TZW4 Friday Night Live kwenda 15678
2. Mkasi – EATV Andika TZW4 Mkasi kwenda 15678
3. Planet Bongo – EATV Andika TZW4 Planet Bongo kwenda 15678
4. Uswazi – EATV Andika TZW4 Uswazi kwenda 15678

5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
1. Juma Kaseja – Yanga Andika TZW5 Kaseja kwenda 15678
2. Mrisho Ngassa – Yanga Andika TZW5 Ngassa kwenda 15678
3. Mbwana Samatta – TP Mazembe Andika TZW5 Samatta kwenda 15678
4. Francis Cheka ¬ Andika TZW5 Cheka kwenda 15678

6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
1. Nisher Andika TZW6 Nisher kwenda 15678
2. Adam Juma Andika TZW6 Adam kwenda 15678
3. Nick Dizzo Andika TZW6 Nick kwenda 15678
4. Mecky Kaloka Andika TZW6 Mecky kwenda 15678

7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
1. My Number – Diamond Andika TZW7 My Number One kwenda 15678
2. Jikubali – Ben Pol Andika TZW7 Jikubali kwenda 15678
3. Mirror – Baby Andika TZW7 Baby kwenda 15678
4. Love Me – Izzo Bizness f/ Barnaba & Shaa Andika TZW7 Love Me kwenda 15678

8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
1. Amani ya Moyo – Feza Kessy Andika TZW8 Amani kwenda 15678
2. Closer – Vanessa Mdee Andika TZW8 Closer kwenda 15678
3. Sugua Gaga – Shaa – Andika TZW8 Sugua Gaga kwenda 15678
4. Yahaya – Lady Jaydee – Andika TZW8 Yahaya kwenda 15678

09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
1. Jacob Stephen aka JB Andika TZW9 JB kwenda 15678
2. King Majuto Andika TZW9 Majuto kwenda 15678
3. Hemedy Suleiman – Andika TZW9 Hemedy kwenda 15678
4. Salim ‘Gabo’ Ahmed Andika TZW9 Gabo kwenda 15678

10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
1. Elizabeth ‘Lulu’ Michael Andika TZW10 Lulu kwenda 15678
2. Jacqueline Wolper ¬ Andika TZW10 Wolper kwenda 15678
3. Shamsa Ford Andika TZW10 Shamsa kwenda 15678
4. Wastara Juma – Andika TZW10 Wastara kwenda 15678

11. FILAMU INAYOPENDWA
1. Foolish Age –Andika TZW11 Foolish Age kwenda 15678
2. Bado Natafuta – Andika TZW11 Foolish Age kwenda 15678
3. Shikamoo Mzee – Andika TZW11 Shikamoo Mzee kwenda 15678
4. Ndoa Yangu – Andika TZW11 Ndoa Yangu kwenda 15678

KUHUSU TUZO ZA WATU

Tuzo za watu Tanzania ni tuzo za aina yake, zilizoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini mahsusi kwaajili ya kuwapa mashabiki wa muziki, filamu, michezo na burudani, jukwaa huru kuwachagua wanaowapenda na kuwakubali katika vipengele vinavyoainishwa na tuzo hizi.
Tuzo hizi zitakazokua za kwanza kwa mwaka 2014, zinatarajiwa kuendeshwa kila mwaka.

Tuzo za watu zinalenga kuanzisha mchakato wa wazi na huru wa utambuzi wa watu wenye umuhimu na michango mahsusi katika nyanja mbalimbali,wanaochaguliwa moja kwa moja na wananchi wenyewe. Tuzo hizi zitatumika kuanzisha urithi utakaoleta hatua mpya ya heshima kwenye jamii yetu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents