Burudani

Mzozo wa kampuni 2 zinazogombania umiliki wa nyimbo za Bob Marley wamalizika

Kampuni ya Cayman Music imeshindwa katika mvutano wa kisheria juu ya umiliki wa baadhi ya nyimbo za hayati Bob Marley huko London, Uingereza.

bob-marley

Kampuni hiyo ambayo iliwahi kuuza haki za umiliki wa baadhi ya nyimbo za Bob Marley mwaka 1992 kwa kampuni nyingine ya Blue Mountain Music, imeshindwa kurejesha umiliki wa nyimbo ilizokuwa ikizidai.

Jaji katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, ukiwemo wimbo uliopata umaarufu ‘No Woman, No Cry’ kuwa haina haki nazo tena.

Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992.

Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents