BurudaniHabari

Moe Tekniks kurudi kimya kimya!

Jay MoeMsanii aliye makini ktk miondoko hii ya Bongo Flava kutoka kundi kongwe la ‘Wateule’,Jay Moe a.k.a ‘Moe Tekniks’ a.k.a ‘Mawazo’ amekamilisha albam yake ya tatu itakayokwenda kwa jina la ‘Kimya Kimya’.

Jay MoeMsanii aliye makini ktk miondoko hii ya Bongo Flava kutoka kundi kongwe la ‘Wateule’,Jay Moe a.k.a ‘Moe Tekniks’ a.k.a ‘Mawazo’ amekamilisha albam yake ya tatu itakayokwenda kwa jina la ‘Kimya Kimya’.

Akiteta na kachero wetu hivi karibuni,Moe alisema albam hiyo iliyomchukua muda na gharama kubwa kuitengeneza…..itakuwa na track 10 na kuzitaja kwa majina kuwa ni;Uko tayari,Matatizo yetu,Tingisha,Ni wewe tu,Mpenzi wa Mjini,Watu wewe,Mungu Nisamehe,Kwenye kila Jamii,Baba na Mama pamoja na Kimya Kimya.

Moe alisema ktk albam hii amedhamiria kuwaletea wapenzi wa muziki wake ladha tofauti na ndio maana ameshirikisha maproducer wakubwa kutoka Kenya na Tanzania ktk kufanikisha hilo.

Alizitaja baadhi ya studio alizofanyia kazi kuwa ni Bongo Records,Serious Records,Soundcrafters ..zote za Bongo na Blue Zebra,Ark Angel na Andaki studio za nchini Kenya.

Baadhi ya wasanii walioshirikishwa kwenye albam hiyo ni Banana Zorro,Ngwair,Black Rhino,TID,KLyinn,Kundi la Necessary Noice pamoja na Kalamashaka kutoka nchini Kenya.

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents