Morocco na Tanzania zitashirikiana kimuziki zaidi, asema Meneja wa msanii aliyeshinda tuzo ya Afrima 2016 (Dj Van)
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2016/11/b760a28e-12f6-4cd0-9a0c-dbf168647b6b.jpg)
Meneja wa Dj maarufu wa nchini Morocco, DJ Van, amesema ushirikiano ulioanzishwa kati ya nchi yake na Tanzania baada ya mfalme wao Mohammed V kuja nchini hivi karibuni, una nafasi nzuri kwa wasanii wa nchi hizo kushirikiana pia.
![b760a28e-12f6-4cd0-9a0c-dbf168647b6b](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2016/11/b760a28e-12f6-4cd0-9a0c-dbf168647b6b.jpg)
Morocco ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na wasanii wakubwa na waliofanikiwa zaidi katika nchi za Kaskazini mwa Afrika. Meneja huyo, Janatte Haddadi, ameiambia Bongo5 kuwa baada ya kusikia taarifa kuwa wananchi wa Morocco wanaweza kuja Tanzania bila visa, walifurahi na kwamba watakuja kwa wingi.
“Sanaa na utamaduni huwaweka watu karibu, hivyo kama tutaweza kufanya kitu na Diamond bila shaka, itafungua connection kati ya Tanzania na Morocco,” alisema Haddadi.
“Itafungua milango kwa watu katika nchi yenu na kwa watu wangu pia,” ameongeza.
![01bb44ae-343a-402f-8169-f5b5b278ab62](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2016/11/01bb44ae-343a-402f-8169-f5b5b278ab62.jpg)
Haddadi amedai kuwa ni muhimu sasa kukawepo na ukaribu wa kumuziki katika nchi za Afrika Kaskazini na zingine za Kusini, Mashariki na Magharibi.