Movie Star Scouting

Movie Star Scouting
Kampuni inayokuja juu kunako tasnia ya filamu Bongo, Tollywood Movies,
imeandaa shindano la kijanja ‘Movie Star Scouting’ ambalo litakuwa
linaibua vipaji vya waigizaji chipukizi nchi nzima na kuviendeleza
kupitia filamu mbalimbali itakazokuwa inaziandaa na kuwafanya star

Kwa mujibu wa msimamizi wa ishu hiyo kutoka Tollywood, Hamie Rajab, shindano hilo linatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kuishirikisha mikoa yote nchini ambapo washiriki watatakiwa kununua fomu za ushiriki zitakazotolewa na kampuni hiyo na kuzijaza kabla ya kufanyiwa usaili.

“Washindi watakaopatikana mikoa watakuja Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki fainali kubwa ambapo washindi wawili wa juu watapata nafasi ya kushiriki katika filamu zinazoandaliwa na Kampuni ya Tollywood ikiwemo filamu mpya ya ‘Siku za Mwisho za Uhai Wangu’ ambayo pia itawashirikisha mastaa kama Ray, Kanumba, Johari na Jokate,” alisema Hamie.

Aidha Hamie, ambaye ni mwandishi mkongwe wa filamu za Kibongo, alisema kwamba fomu za kushiriki zitauzwa kwa shilingi 5,000. Kampuni ya Tollywood ndiyo watengnezaji wa ‘muvi’ zilizotamba sokoni kama Fake Pastors na From China With Love. Kama wewe unadhani una kipaji cha kuigiza huu ndiyo wakati wako wa kuwa staa wa filamu Afrika. Kaa tayari kwa taarifa kamili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents