Burudani

Msanii wa Namibia Chikune amemtaja msanii wa Bongo Fleva anayekubalika zaidi nchini humo

Mshindi wa tuzo ya Afrimma 2016 kwenye kipengele cha Best Female, Southern Africa, Chikune kutoka Namibia amefunguka kwa kumtaja msanii wa Bongo Fleva anayekubalika zaidi nchini humo na sababu ya wasanii wa nchi hiyo kutofanya vizuri kwenye tuzo kubwa za Afrika.

13256693_640787786069078_1704542408_n

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5, “Diamond anakubalika zaidi kwa sababu ni mburudishaji, mfanyabiashara na amefanikiwa kuwafanya mashabiki kufurahia muziki wake bila ya kujali lugha anayoitumia.”

Akiongea kuhusu kutofanya vizuri kwa wasanii wa nchi hiyo kwenye tuzo kubwa za Afrika, amesema, “Namibia ni kama bwawa la vipaji vya muziki, ila kuna mapungufu yanayotokana kwenye soko la muziki la ndani lililofunikwa na kivuli cha soko la muziki la Afrika Kusini.”

Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Kapana’ aliouachia mwezi April mwaka huu.

https://youtu.be/mrsqttHFe6Q

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents