Burudani

Mshindi wa Wikienda Music Search (WMS) kufanyiwa hiki na Wanene Entertainment

Studio za Wanene Entertainment za jijini Dar es salaam zitamfanyia video na audio msanii, Frank Mgogosi ambaye wiki hii aliibuka mshindi kwenye Shindano la Wikienda Music Search (WMS) lililoandaliwa na Gazeti la Ijumaa Wikienda.

Mshindi wa shindano hilo Frank Mgogosi (kushoto) akisalimiana na mshindi wa pili Allen Venance

Mshindi huyo alikuwa anachuana na msanii mwenzake kutoka Ilala, Allen Venance. Usaili huo ulifanyika katika studio za Wanene Entertainment iliyopo mikocheni jijini huo.

Mratibu wa mashindano hayo kutoka Gazeti la Ijumaa Wikienda, Gabriel Ng’osha (katikati) akizungumza na wasanii hao baada ya mshindi kupatikana.

Usaili huo ulisimamiwa na maproduzya watano akiwemo Shentee Murozy wa Black Studio, King Luffa, Dr. Reggy, Goncher na Humphey kutoka Zimbambwe.

Majaji, mshindi wa kwanza na wapili wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya ofisi ya Wanene.

Jumla ya wasanii 60 waliweza kushiriki mashindano hayo ambayo yalikuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa wasanii hao.

Mshindi wa shindano hilo, Mgogosi ameishukuru Studio ya Wanene, Black na Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa kuwasaidia wasanii chipukizi na kuwashauri watu kusoma kwa bidii Magazeti ya Global Publishers kwani yana fursa nyingi ikiwemo bahati nasibu kubwa kabisa ya Shinda Nyumba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents