Habari

Wanachuo wa DUCE wajitolea kufundisha masomo ya sayansi katika shule za sekondari Temeke

Wanachuo wa Dar Es Salaam University College of Education (DUCE), wapatao 30 wamejiunga na kujitoa kufundisha Masomo ya Sanyansi wenye Shule za Sekondari za Wilaya ya Temeke jijini Dar.

Mwanafunzi wa chuo cha Dar Es Salaam University College of Education (DUCE), Emijidius Cornel (kushoto) ambaye ndio mwanzilishi wa harakati hizo akiwa kwenye moja kati ya matukio ya kijamii ambayo huwa anafanya.

Wanachuo hao wamechukua uamuzi huo ili kuwasaidia wanafunzi ambao wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali kwenye masomo yao ya sayansi.

Mwanzilishi wa harakati hizo, Emijidius Cornel amesema wamedhamilia kujitoa kwa hali na mali ili kuwasaidia wanafunzi wa Wilaya ya Temeke, ambapo katika baadhi ya shule ambazo wameenda kufundisha wamekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo wanafunzi kukosa msingi wa masomo ya sanyansi tangu vidato vya awali.

“Nashukuru mimi na wanachuo wenzangu ambao wameungana nami katika harakati hizi za kuwasaidia wadogo zetu kuhakikisha wanaweza kufanya vizuri kwenye masomo yao.

“Tumekutana na changamoto nyingi kwenye baadhi ya shule ikiwemo ukosefu au upungufu wa walimu wakutosha wa masomo husika, wanafunzi kukosa msingi mzuri wa masomo tangu awali.

“Changamoto nyingine ni umbali wa sisi wanachuo kuweza kuzifikia shule husika kutokana na kutokuwa na usafiri wa uhakika zaidi ya kujichanga wenyewe.

“Wito wangu kwa wadau ambao wanaweza kuungana na sisi katika mchakato huu tunawakaribisha kwa namna yoyote ile, tuko tayari kushirikiana nao,”alisema Cornel.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents