Habari

Muigizaji mrembo wa Bollywood Jiah Khan ajiua, aliigiza filamu maarufu ‘Ghajini’

Muigizaji mrembo wa Bollywood, Jiah Khan amepatikana akiwa amekufa nyumbani kwake jijini Mumbai, India. Mama yake Khan anasema aliukuta mwili wa binti yake ukiwa unaning’ania jana usiku.

Jiah Khan

Uchunguzi wa mwili wake unafanyika ili kubaini chanzo cha kifo chake na polisi wameendelea kupata maelezo kutoka kwa majirani lakini asilimia nyingi zinaonesha kuwa muigizaji huyo alijiua.

Jiah alikuwa ametokea mjini Hyderabad kwenye usaili wa filamu. Inadaiwa kuwa alikuwa amekosana na mpenzi wake Suraj Pancholi hali iliyomuumiza sana na pia alikuwa akihangaika kurejea tena kwenye filamu bila mafanikio.

jia1a

Muigizaji huyo mwenye miaka 25 alianza kupata umaarufu mwaka 2007 kwenye filamu ya Amitabh Bachchan, na aliendelea kuigiza na mastaa wakubwa wengine wakiwemo Aamir Khan na Akshay Kumar.

jiah-khan-1

Jiah Khan alizaliwa New York na kukulia London kabla ya kuhamia Mumbai kuendelea na uigizaji wa filamu za Bollywood.

jiah_khan02_10x7

Kifo chake kimesababisha mshtuko mkubwa kwenye tasnia ya filamu nchini India.

Jiah Khan aliigiza kwenye filamu ya Nishabd, Amitabh Bachchan na , Ghajini ambayo muigizaji mkuu alikuwa Aamir Khan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents