Michezo

Jose Mourinho asaini mkataba wa miaka minne kujiunga tena na Chelsea

KOCHA Jose Mourinho jana amekutana na viongozi wa Chelsea kukamilisha mpango wa kurejea tena Stamford Bridge.

jose

Taarifa rasmi zilithibitishwa jana jioni kuwa Mourinho amesaini Mkataba wa miaka minne hii ikiwa ni mara ya pili kwa Mourinho kufanya kazi klabu hiyo ya London.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 50 tayari ataanza kazi Chelsea wiki hii ambapo mechi yake ya kwanza ikitarajiwa kuwa kwenye mtanange wa matayarisho nchini Thailand dhidi ya Singha All Stars XI, katika ziara ya huko Malaysia na Indonesia.

Baada ya hapo The Blues wataenda Marekani kwenye michuano ya International Champions Cup itakayohusisha timu za Real Madrid na Inter Milan, pia Everton, Juventus, AC Milan, Valencia na LA Galaxy.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents