MUSOMA: Polisi afa maji wakati akimkimbiza mtuhumiwa wa ujambazi

Musoma. Askari polisi, Isaya Kawogo amefariki dunia baada ya kuzama katika Ziwa Victoria wakati akimkimbiza mtuhumiwa wa ujambazi.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Mei 28, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu akibainisha kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mwisenge manispaa ya Musoma.

Amesema askari huyo pamoja na wenzake wakiwa doria walikutana na mtuhumiwa huyo na kuanza kumkimbiza.

“Yule mtuhumiwa alijitosa ziwani na askari aliamua kumfuata huko huko ziwani lakini akiwa katika harakati za kumkamata alinasa kwenye nyavu na kuzama. Mtuhumiwa alifanikiwa kuimbia,” amesema kamanda huyo.

Related Articles

Back to top button