Habari

Mvua zinazoendelea kunyesha Dar zasababisha baadhi ya barabara kufungwa

Athari za mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam zimeanza kuonekana baada ya kusababisha baadhi ya barabara katika jiji hilo kufungwa kutokana na kujaa kwa maji.

Baadhi ya barabara ambazo zimefungwa ni Morogoro Road eneo la Jangwani, Kinondoni Mkwajuni, Kawawa eneo la Kigogo pamoja na Kibada kuelekea Kisarawe kutokana na kuvunjika kwa daraja na kukata mawasiliano.

Watu mbalimbali waliopo mjini wameshauriwa kutafuta barabara mbadala za kurejea majumbani huku wakitakiwa kuwa makini pindi wanapopita katika madimbwi ya maji.

Eneo la Jangwani lilifungwa tangu jana kutokana na kiwango cha maji kuongezeka hivyo kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara hiyo.

Kufungwa kwa barabara hiyo kumeleta athari kwa wananchi hasa wale ambao wanatumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka ambayo yamekuwa yakipita katika njia hiyo kuelekea mjini Posta na Kariakoo.

Aidha barabara ya Kinondoni Mkwajuni imefungwa kwa sababu ya wingi wa maji yanayopita juu ya barabara katika bonde hilo ambayo yanahatarisha usalama wa watumiaji.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents