Habari

Mwaka mpya 2022 wakabiliwa na ‘tsunami’ ya Corona

Mamilioni ya watu kote ulimwenguni wanajiandaa leo kwa maadhimisho ya Mwaka Mpya yaliyowekewa vizuizi vikali.

COVID in Europe: Countries see record daily cases amid uncertainty over  Omicron impact | Euronews

Idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona yanayochochewa na kirusi cha Omicron imelifanya shirika la Afya Ulimwenguni – WHO kuonya kuwa tsunami ya Covid inatishia kuelemea mifumo ya afya.

Kirusi kipya cha Omicron kimesababisha ongezeko kubwa kabisa la maambukizi katika siku za karibuni nchini Marekani, Uingereza, Ufaransa na nchi nyingine za UIaya, na kuzilazimu serikali kutangaza tena vizuizi.

Kuanzia Ugiriki hadi Mexico, kutoka Barcelona hadi Bali na kote Ulaya, mamlaka zimefuta au kupunguza mikusanyiko ya umma ama kwa kufunga au kuweka vizuizi kwenye kumbi za starehe za usiku.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ana wasiwasi mkubwa kuwa kirusi cha Omicron, ambacho kinaambukiza zaidi na kusambaa kwa kasi kwa wakati mmoja na kirusi cha Delta, kinasababisha idadi kubwa ya maambukizi ya kiwango cha tsunami.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents