Michezo

Mwakinyo apanda viwango vya ubora duniani

Bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amepanda katika viwango vya ubora duniani kutoka nafasi ya 24 hadi ya 13 akiwa na alama 23.48 uzito wa Super Welter.

Mwakinyo amepanda hadi nafasi hiyo baada ya kumtwanga Mnamibia, Julius Indongo kwa KO na kufanikiwa kuutetea ubingwa wake wa Afrika (ABU) siku ya Ijumaa Septemba 3 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Bondia huyo namba moja Tanzania na Bara la Afrika uzito wa Super Welter mwenye nyota nne alimpiga Indongo bingwa wa zamani wa WBO na WBC katika raundi ya nne (4) kwenye pambano la raundi 12. Rekodi hizo zinaandikwa na mtandao maarufu wa Boxing duniani, BoxRec.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents