Habari

Mwalimu Nyerere ni mfano wa kuigwa – Rais Magufuli

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanznia Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kuiga mema yote aliyokuwa akifanya muasisi wa Taifa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere.

Dkt. Magufuli ametoa rai hiyo katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ,Kumbukumbu ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius K. Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika katika uwanja wa Amaan na amesema kuwa kiongozi huyo alikuwa ni mtu mwenye uzalendo,apenda Amani, haki, usawa na mwenye maono.

Vile vile Rais Magufuli amesisitiza serikali yake kwa upande wa Bara na Visiwani kuwa hawatoacha kukimbiza Mwenge huo kwani umekuwa na tija kwa kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Mbio za Mwenge wa Uhuru zilianza rasmi mwezi wa nne tarehe mbili Mkoni Katavi na zimehitimishwa leo katika Mkoa wa Mjini Magharibi chini ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahamud.

Pia mbio hizo za Mwenge zimezindua miradi 15, ikiwemo miradi ya :- Afya, Elimu, Maji safi na salama, Viwanda, Huduma kwa jamii na mingineyo. Kwa upande wiki ya Vijana , Rais Magufuli amewataka vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya kwani yanaharibu nguvu kazi.

Baadhi ya picha za matukio.


Na Salumu Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents