Habari

Mwanaharakati wa kupinga ndoa za utotoni Rebeca Gyumi ashinda tuzo ya Umoja wa Mataifa

Mwanaharakati wa Tanzania wa kupinga ndoa za utotoni, Rebeca Gyumi ameshinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Malengo ya dunia katika kipengele cha mabadiliko ya kijamii.

rebecca

Gyumi ambaye ni mwanasheria na mtangazaji wa TV, alikabidhiwa tuzo hiyo Jumanne hii jijini New York Marekani mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia waliopo jijini humo kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa.

22

“Angelique Kidjo aliniita akaniambia “nataka nikukumbatie kwa nguvu,natamani wasichana wa Afrika wengi wawe Kama wewe”. Kwakweli ni heshima kubwa nimepewa,” ameandika Gyumi.

untitled
Mtangazaji wa CNN, Christine Amanpour ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo

Mwaka huu Gyumi kupitia taasisi yake ya Msichana Initiative, alifungua shauri katika mahakama kuu ya Tanzania kupinga vipengele viwili vya sheria ya ndoa vinavyotoa mwanya wa mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kwa kibali cha mahakama na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.

Alifungua na kushinda shauri hilo ili kuondokana na ongezeko la ndoa za utotoni lililoshamiri katika mikoa ya Kaskazini hususani katika mikoa ya Shinyanga na Dodoma.

Hata hivyo serikali ilipinga hukumu hiyo iliyotolewa Julai 8.
Gyumi ambaye hutangaza kipindi cha Femina, amehusika kwenye kampeni nyingi za kujitolea kuhusu masuala ya kijamii.

333

Nov, 2013, aliteuliwa na ubalozi wa Marekani kuhudhuria ‘International Visitors Leadership Program (IVLP)’ uliohusisha vijana wenye dalili za kuwa viongozi wazuri wa baadaye.

Rebeca ni makamu wa rais wa Tanzania Association of US State Alumni (TUSSAA), balozi wa Tanzania wa Trek4Mandela na pia mjumbe wa mradi wa OYE wa SNV-Netherlands.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents