Habari

Mwasiti kuja na album yenye nyimbo za Jazz

Mwasiti anajipanga kulikuza jina lake kimataifa kwa kufanya muziki usio maarufu sana katika nchini za Afrika – Jazz.

10953589_343631809156356_735313203_n

Muimbaji huyo amedai kuwa yupo jikoni kuandaa album itakayokuwa na nyimbo za jazz peke yake.

Mwasiti amedai kuwa atawashirikisha watayarishaji mbalimbali wa muziki nchini kuandaa album hiyo . Miongoni mwa maproducer hao ni pamoja na Nash Designer na Tudd Thomas.

Muziki wa Jazz si maarufu sana kwenye masikio ya Watanzania wengi na ni miongoni mwa aina ya muziki mgumu zaidi kuufanya na huhitaji elimu nzuri ya muziki kuweza kuumudu.

Muziki huo ulianzia kwenye jamii za Wamarekani weusi mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 21.

Wakati huo huo leo ni siku ya kuzaliwa ya Mwasiti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents