Habari

Mwigulu Nchemba ala sahani moja na walimu waliomjeruhi mwanafunzi Mbeya

UPDATES: Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako amewafukuza chuo walimu waliohusika na kumpiga mwanafunzi wa kidato cha 3, Mbeya Day Sec. School

Baada ya kusambaa kwa video inayowaonesha walimu takriban watano wakimpiga bila huruma mwanafunzi wa shule ya kutwa ya Mbeya, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amechukua hatua.

14026642_245715935822573_429135586_n

Kupitia Instagram, Mwigulu amesema kuwa polisi Mbeya wanaendelea kuuhoji uongozi wa shule hiyo.

Haya ni maelezo yake:

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo. Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile.

Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo. MWIGULU Nchemba, W MNN

Kitendo hicho kimesababisha hasira kali kwa wananchi wanaotaka kuwepo adhabu kali kwa walimu hao.

https://youtu.be/l2fnEaInIrw

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents