Burudani

Mzee Chilo adai runinga zilisababisha kupotea tamthilia za nyumbani

Msanii wa filamu, Mzee Chilo amedai wamiliki wa runinga nchini ndio waliosababisha kupotea kwa tamthilia za nyumbani kwa kuzikwepa na kuonesha za kigeni.

Mzee Chilo akizungumza jambo na watoto

Muigizaji huyo ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Pilipili Entertainment, ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo imesababisha wazalishaji wa filamu nchini kukaa na kazi zao ndani bila kuwa na sehemu za kuzipeleka.

“Kilichopoteza tamthilia zetu ni runinga zetu, wakawa wanaamua kuonesha tamthilia za kigeni sijui kwao ndio zilikuwa rahisi?” amesema Chilo.

“Lakini sasa hivi naona wameanza kurudi na kutuona sisi ni wa muhimu, wanajali kazi zetu. Hii italeta makubwa katika tasnia yetu kwa sababu wasanii wanajengwa na tamthilia, hao wote wanaotajwa akina Ray, Kanumba na wengine wametokana na tamthilia kwa sababu tamthilia unaangalia nyumbani kwako na familia yako,” ameongeza.

Pia Mzee Chilo amesema baada ya kupata serikali inayowasikiliza wananchi wake ana imani kila kitu kitaenda sawa mwaka 2016.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents