Habari

Utafiti: Upungufu wa nguvu za kiume huongeza hatari ya kupoteza maisha mapema kwa asilimia 70

Ni kitu kinachofedhehesha ambacho huathiri shughuli ya mwanaume kitandani.

Anorgasmia

Lakini sasa, wanasayansi wameonya kuwa upungufu wa nguvu za kiume ambao kitaalam hujulikana kama (erectile dysfunction) unaweza kuwa na athari katika maisha ya mwanaume.

Wamebaini kuwa wanaume wenye matatizo hayo wana asilimia 70 ya kufa mapema. Hii ni kwasababu tatizo hilo lina uhusiano na magonjwa ya moyo.

Kwa kawaida, upungufu wa nguvu za kiume umekuwa ukichukuliwa kama kitu kinachoathiri watu wenye umri mkubwa. Hata hivyo, wanasayansi wamedai kuwa asilimua 20 ya wanaume walio chini ya miaka 40 wameathirika na tatizo hilo.

Ilikuwa imeshabainika kuwa tatizo hilo linahusishwa na mambo yanayosababisha magonjwa ya moyo yakiwemo shinikizo la damu, unene, kisukari na uvutaji wa sigara.

Utafiti huo ulifanywa kwa wanaume 1,790 wa umri kuanzia miaka 20 hadi 85 walioshiriki kwenye survey ya mwaka 2003-2004 nchini Marekani.

Waliunganisha data hizo na vyeti vya vifo kutoka December 21, 2011.

Wanasayansi walibaini kuwa watu 557 walikuwa na tatizo hilo.

Baada ya kuwafuatilia kwa takriban miaka minane, walibaini kuwa 244 walikuwa wamefariki.

Soma zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents