Habari

Mzee Majuto hali yake si shwari, alazwa tena ICU Muhimbili

Afya ya mchekeshaji mkongwe nchini Tanzania, Mzee Majuto bado sio nzuri kwani amelazwa tena katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  Jumanne ya wiki hii.

Image result for mzee majuto
Mzee Majuto

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha ndiye aliyethibitisha taarifa hizo za kulazwa kwa Mzee Majuto.

Hii inakuwa mara ya pili kwa mchekeshaji huyo kulazwa katika Hospitali ya Muhimbili kwani mapema mwaka huu alilazwa Hospitalini hapo kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi.

SOMA ZAIDI – Mzee Majuto arejea nchini akitokea India

Related Articles

19 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents