Burudani

Nandy afikisha watazamaji mil 100 youtube, msanii wa pili wa kike Tanzania baada ya Zuchu

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nnady alimaarufu The African Princes @officialnandy amekuwa msanii wa Pili Afrika Mashariki na kati kufikisha jumla ya watazamaji Milioni 100 kwenye Mtandao wa kusambaza muziki Ulimwenguni #YouTube.

Nandy amefikisha idadi hiyo kwenye mtandao huo na kuvuna Subscribers zaidi ya 723,000. Nandy anakuwa msanii wa Pili kufikia idadi hiyo ya kutazamwa huku namba moja ikishikwa na @officialzuchu kutoka lebo ya #WCB mwenye 141,067,941 views huku Nandy akiwa na 100,925,428 views.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nandy amewashukuru mashabiki wake kwa kuandika “Views 100M+ on @youtube Haikua kazi rahisi, Nashukuru kwa Watu wote waliofanikishwa kupiga hatua hii kubwa katika mziki wangu

Huu ni Mwanzo mpya wa kupambana na kufika mbali zaidi na kupeperusha bendera ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents