Burudani

Nay wa Mitego adai hana mpango wa kuoa tena

Msanii Nay wa Mitego amesema kwa sasa hana mpango wa kuoa na wala hafikirii kuoa, licha ya kuwa na watoto ambao wanahitaji malezi ya mama.
Chagga-na-Nay

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatatu hii, Nay alisema kuwa kwa sasa hayuko kwenye mahusiano yoyote, na suala la kuoa kwake ni suala zito, hivyo hawezi kukurupuka na kuchukua uamuzi wa kuoa.

“Kusema kweli kabisa nimeulizwa swali ambalo sijaulizwa muda mrefu, na nikiulizwa huwa nalikwepaga, kufuatana na mahusiano ambayo nimekuwa nayo katikati, namshukuru Mwenyezi Mungu amenijalia watoto, for this time nikisema nizungumzie kuhusu ndoa nitadanganya, mi sifikirrii kabisa kuhusu kuoa for this time, kwa bahati mbaya au mzuri mi sipo kwenye mahusiano, sitaki kukurupuka, unajua ukifunga ndoa kwa sisi, mi ni mkristo hiyo ndo nitolee, yani hapo ndo umejicomit umeshaingia kwenye 18 ambazo huwezi kuzipangua tena, sifikirii kuoa, siwazi na sidhani kama nina huo mpango”, alisema Nay wa Mitego.

Pia Nay wa Mitego amekiri kuwa na mahusiano na Stella ‘Chaga Baby’ ambaye anaishi Marekani, lakini umbali uliopo kati yao ndio chanzo cha wao kutokuwa pamoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents