Burudani

Nay wa Mitego adai kuingiza zaidi ya shilingi milioni 80 kwa muziki mwaka huu pekee

Rapper Nay wa mitego amefunguka kwa kusema kuwa ndani ya mwaka huu ameingiza zaidi ya shilingi milioni 80 kutokana na muziki pamoja na baadhi ya matangazo madogo madogo aliyoyafanya.

Nay Wa Mitego akiimba kwa hisia katika serengeti fiesta Mtwara.
Akizungumza na Bongo5, Nay alisema tangu ameanza kufanya muziki hajawahi kufulia.

“Kama kujenga nilishajenga tangu hata sijaanza kufanya muziki,na sasa hivi nimekuwa nikijitaidi kufanya muziki wangu kama ndio mtaji wa maisha yangu ndio maana hata kuna baadhi ya deal za matangazo nimekuwa nikizikataa kutokana na bei.Kama mtakumbuka nilhitajika niwe judge katika mashindano ya BSS lakini nilishindwa nao kutokana niliona haina maslahi kwangu,” alisema Nay.

“Kuna kampuni ya simu ilinipigia simu kunihitaji mimi niwe balozi na kufanya baadhi ya matangazo ila bado hatujafika muafaka ,tupo kwenye makubaliano ya bei.Kama ningekuwa msanii njaa ungenikuta kwenye matangazo,lakini nahitaji kama tukikubaliana na mimi ninufaike vizuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents