Kampuni ya Singapore kuwekeza dola bilioni 1.3 kwenye visima vya gesi nchini
Kampuni ya Pavilion Energy Pte, ya nchini Singapore itawekeza dola bilioni 1.3 kwaajili ya kumiliki asilimia 20 ya umiliki wa visima vitatu vya gesi nchini Tanzania.
Mwenyekiti Mtendaji wa Pavilion Energy Pte, Seah Moon Ming
Pavilion Energy, inayomilikiwa na Temasek Holdings Pte, iliingia kwenye makubaliano na kampuni ya Ophir Energy Plc (OPHR), ambayo inamiliki asilimia 40 ya cubic feet trilioni 15 za gesi kwenye visima vitatu, ilisema jana kwenye maelezo yake.
“Uendelezaji wa gesi asilia nchini Tanzania una faida kubwa, si tu kwa Pavilion Energy lakini pia kwa Singapore na Asia,” Hassan Marican ambaye ni mwenyekiti wa Pavilion, alisema kwenye maelezo yake.
Kampuni ya Berkshire, ya Uingereza inamiliki asilimia 60 ya visima hivyo.
Source: http://www.bloomberg.com