Burudani

Nayaandika haya kutoka moyoni mwangu Young Dee – Max Rioba

Ikiwa ni wiki kadhaa toka rapper Young Dee akiri kutumia Madawa ya kulevya na kuwaomba radhi mashabiki wake, uongozi wa rapper huyo umeendelea umuombea dua msanii huyo ili asirudi tena katika janga hilo.
Young DEE
Young Dee akiwa na Max Rioba

Rapper huyo ambaye anapendwa kwa style yake ya kuchana, alitumia Madawa ya kulevya kwa muda wa mwaka mmoja hali ambayo ilimfanya apoteza mwelekeo wake.

Mkurugenzi wa label ya ‘MDB’ ambayo inamsimia rapper huyo, Max Rioba, kupitia instagram yake ameandika haya kuhusu rapper huyo.

“Namwomba Maulana akusimamie mwanangu uendelee kufanya vizuri na uishangaze dunia na walimwengu wakaao ndani yake. Shikilia hapo hapo uliposhikilia, utafanikiwa tu,” alisema Max. “Muamini Mungu, muombe yeye akupe ujasiri wa kuushinda moyo kila unapohisi unakaribia kuanguka. Akupe akili za utambuzi uone kisiki kilichoko mbele yako kabla hujajikwaa. Awabariki wale wote wanaochukia maamuzi yako na kuwabariki zaidi wanaokuunga mkono, nayaandika haya kutoka moyoni mwangu Dee. Naamini una nyota inayoweza kung’aa hadi mbali sana,”

Aliongeza, “Najua wako watu wengi sana wanaochukia sana hii movement, Lakini kamwe usiwasikilize. Uliamua mwenyewe kuanguka, ukaamua mwenyewe kuamka. Amua mwenyewe kushikilia msimamo wa mabadiliko yako. Kuna kijana mwingine anaepitia mambo kama uliyoyapitia anasubiri aone umesimama imara naye apate nguvu za kunyanyuka. Fight for yourself, work it out, force your damn self to stay up tight, to stay on top. Then uone utakavyofanikiwa. You’re not a star Dee, you’re a megastar, bigger than a superstar!!! Hands Up y’all. I’m done,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents