Habari

Nchi nyingine ya pili barani Afrika yahalalisha kilimo cha bangi

Kwa nchi za Afrika ukiitoa Lesotho ni kosa kisheria kulima au kutumia Bangi hii ni kutokana na maelezo kuwa zao hilo ni moja ya aina ya madawa ya kulevya.

Govt legalises mbanje farming
David Parirenyatwa

Sasa Zimbabwe nayo inakuwa ni nchi ya pili barani Afrika kuruhusu zao hilo lilimwe na kutumiwa kama tiba na matumizi mengine ya kisayansi.

Kwa mujibu wa gazeti la The Herald la nchini Zimbabwe limeeleza kuwa Waziri wa afya nchini humo, David Parirenyatwa amechapisha baadhi ya vifungu vya sheria vinavyowaruhusu watu na makampuni kupewa leseni ya kufanya kilimo cha bangi.

Kwa vifungu hivyo watu wa nchi hiyo sasa wanaweza kulima na kutumia bangi,ambapo leseni ya kilimo hicho itadumu kwa miaka mitano.

SOMA NA HII – Lesotho yawa nchi ya kwanza barani Afrika kuhalalisha kilimo cha bangi

Mwaka jana Lesotho ilitangaza ilihalalisha kilimo cha bangi kwa sababu za kibiashara na tiba na wakati wa pendekezo hilo serikali ilisema itaingiza kiasi cha dola milioni 240 kwa mwaka kupitia bidhaa hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents