Michezo

RASMI: Vikosi vya Simba SC na Yanga SC vyatangazwa

Ikiwa ni masaa tu yanasubiriwa kuanza kwa mtanange wa mechi kati ya klabu ya Simba na Yanga kunako dimba la Uwanja wa Taifa, tayari vikosi vya timu zote mbili vimeshatangazwa.

Yanga hao watawakosa wachezaji wao muhimu kama Amis Tambwe na Donald Ngoma ambao wote ni majeruhi huku Simba ikiwa na wachezaji wake wote muhimu ambapo mashambulizi yataongozwa na Emmanuel Okwi na John Bocco.

Klabu ya Simba inaongoza ligi kwa pointi 59 ikifuatiwa na Azam FC wenye pointi 46 na Yanga ni ya tatu kwenye msimamo kwa alama 48.

Hata hivyo Simba imecheza michezo mingi 25 huku mahasimu wao wakiwa na viporo vya mechi mbili (23).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents