Burudani

Ndugu wanamtaka Afande Sele aoe, asema hajapata mwenye mapenzi ya dhati

Afande Sele amesema changamoto kubwa anayokumbana nayo kila akitembelewa na ndugu zake tangu afiwe na aliyekuwa mke wake, Mama Tunda ni kumtaka aoe.

Afande Sele akiwa na watoto wake Mkubwa anaitwa Tunda na mdogo Sanaa
Afande Sele akiwa na watoto wake Mkubwa anaitwa Tunda na mdogo Sanaa

Akizungumza na Bongo5, Afande amesema ameshauriwa mara nyingi suala la kuoa lakini tatizo linakuja jinsi ya kumpata yule mwenye mapenzi kweli.

“Familia yangu sasa hivi imekuwa inazungumzia suala hili, yaani shangazi zangu, baba zangu wamekuwa sana wananitembelea hapa nyumbani na suala la kuoa ndo limekuwa jambo lao kubwa la kunisisitiza. ‘Inakuwaje inabidi ufanye mpango uweze kutafuta mazingira mengine’ wakimaanisha kuoa. Lakini mimi nimefikiria na nimeona ni jambo la msingi lakini sasa bahati mbaya jambo la kuoa si kama kwenda dukani na kusema utaenda tu kuchagua nguo nzuri unaivaa. Kwenye suala la kuoa unatakiwa kabisa ujue ni mtu gani unamuoa na yeye yupo tayari kiasi gani kuishi na wewe.”

“Pia mimi inanipa wakati mgumu kwa sababu nina jina na kama nina jina sio rahisi kumpata anayekupenda kweli, wengine wamependa jina au amependa jinsi ninavyofanya maisha, lakini kwenye moyo wake atakuwa hayupo tayari kwa ndoa. Hili suala jema na mwenyezi Mungu akinijalia nitaoa na kuacha maisha yangu yaendelee kama kawaida,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents