Burudani

Ben Pol azungumzia ndoa na video mpya na Nisher

Ben Pol amesema kama Mungu akimjalia basi huenda akafunga ndoa na mpenzi wake Miss Tanzania namba mbili 2013, Latifa Mohamed.

Ben Pol

Ben Pol ameiambia Bongo5 kuwa ukaribu alionao na Latifa unampa matumaini ya kudumu kwa uhusiano wao.

“Tupo karibu sana, suala la ndoa sijui nisemeje lakini, kama mwanaume kamili tena kwa mila zetu nitaoa tu lakini, tukikubaliana na yeye akawa tayari yaani kila mtu akiwa tayari na akili zetu zikiendana na Mungu akijalia itakuwa hivyo. Pia unajua hii inakujaga automatic,” amesema.

Katika hatua nyingine, Ben Pol amesema anatarajia kufanya video nyingine na Nisher.

“Huu upya ambao nakuja nao ni kuanzia uvaaji, yaani kuna mabadiliko makubwa sana nataka kuja nayo ya kimwonekano. Ndioa maana nimeamua kuachana na kufikiria kutoa wimbo redioni kwanza nataka kwanza video moja tena kwa Nisher na haya mabadiliko yaambatane na wimbo mpya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents