BurudaniDiamond Platnumz

Ne-Yo kutumbuiza Mwanza, May 21

Muimbaji wa Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo, anatarajiwa kutumbuiza jijini Mwanza, May 21.

ne-yo-crop

Atatumbuiza kwenye tamasha kubwa la kila mwaka la Jembeka linaloandaliwa na kituo cha redio cha Jembe FM cha jijini humo.

Hii itakuwa mara ya tatu muimbaji huyo kuja Afrika Mashariki. Ameshatembelea Kenya alikoenda kwenye Coke Studio Afrika mwaka jana na Uganda alikoenda kutumbuiza.

Kwenye tamasha hilo pia, Diamond ambaye mwaka jana alimshirikisha msanii huyo atakuwepo.

Ni hivi karibuni tu kituo hicho kinachofanya vizuri jijini Mwanza kiliwaleta wasanii wa Nigeria, Seyi Shay na Tekno kwenye tamasha la utangulizi la Muzika lililofanikiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents