HabariMichezo

Ngumi zaruhusiwa Zanzibar

Serikali ya Zanzibar imetangaza rasmi kuruhusu mchezo wa ngumi kuanza kufanyika visiwani humo baada ya kupigwa marufuku Januari 12, 1964 na Rais wa kwanza Abeid Aman Karume.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Tabia Maulid Mwita alitangaza uamuzi huo katika kikao cha baraza la wawakilishi baada ya kupata maoni ya wananchi mbalimbali waliohojiwa na kupata baraka za Baraza la Mapinduzi.

Waziri huyo alisema utafiti mdogo uliyofanywa ambapo jumla ya wananchi 5,702 walihojiwa katika mikoa mitano ya Zanzibar na watu 3,614 sawa na asilimia 63.4 walitaka mchezo huo uruhusiwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents