Michezo

Nick Kyrgios afungiwa kucheza tennis wiki nane

Mcheza tennis nambari 14 kwa ubora duaniani Muaustralia Nick Kyrgios amefungiwa kwa wiki nane na kutozwa faini ya dola za kimarekani 25,000 kwa utovu wa nidhamu-ikiwa ni pamoja na kucheza ovyo wiki iliyopita michuano ya Shaghai Masters.

ef166b39061198ee8006d573ba6d2221

Nick ambaye anamiaka 21 amekuwa akigongesha mpira juu ya wavu mara kadhaa katika mchezo aliofungwa Mischa Zverev kwa seti 6-3 6-1 .

Hata ivyo baada kufungiwa ameomba radhi kwa tukio hilo na kusema atafanyia kazi wakati huu akiwa kifungoni.

Wiki iliyopita Muingereza Andy Murray alisema hafikirii kuwa faini pekee itakuwa adhabu tosha.

Mwaka 2015 katika michuano ya kombe la Roger Kyrgios alifungiwa siku 28 na faini ya dola 25,000 baada ya kutoa maneno ya kashfa kwa mpenzi wa Stan Wawrinka.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents